Wednesday, November 9, 2011

Imedondoka, iokote, ipanguse kitu pwani (mdomoni)... Usalama wa afya zetu hasa wasafiri njiani ni mdogo sana





Pichani ni Kijana ambaye ni mfanyabiashara mdogo mdogo maarufu kama MACHINGA katika kituo cha mabasi makubwa mkoani Mara, ambapo pichani anaonekana akirudishia karanga zilizodondoka chini baada ya mfuko kupasuka tayari kwa kuuziwa mteja.

Saturday, March 26, 2011

TAIFA LA KESHO LIMEPOTEZA MATUMAINI... Hii ndio hali halisi ya watoto waishio kwenye mazingira magumu mkoani Mwanza




Moja ya watoto waishio katika mazingira magumu mkoni Mwanza wakiwa wameuchapa usingizi barabarani na katika moja ya mitaro wa kupitisha maji machafu jijini humo. Hali hii inasikitisha kwani hili ndio taifa la kesho ambalo limesha kata tamaa. Baada ya Serikali ya Tanzania kulaumiwa sana, Je, sisi kama jamii tumechukua hatua gani kuliinua Taifa hili la kesho ambalo limepoteza matumaini? Na je baada ya miaka michache ijayo Tanzania itakuwa na vijana wa aina gani... TAFAKARI

Tuesday, March 22, 2011

Kilele cha maadhimisho ya 23 ya wiki ya maji yafanyika kitaifa leo mkoani Mwanza , mgeni rasmi akiwa ni makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal


Makamu wa Rais Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal akihutubia wananchi katika maadhimisho ya 23 ya wiki ya maji yaliyofanyika kitaifa leo mkoani Mwanza, Kauli mbiu ikiwa ni MAJI KWA AJILI YA MIJI: KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI MJINI. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal amesema maadhimisho haya yanatoa fursa kwa kila mmoja wetu kutafakari wajibu wake katika dhana ya matumizi mazuri ya maji na utunzaji mazingira.
Pia Makamu wa Rais hakusita kuzitaja changamoto za utoaji wa huduma ya majisafi na majitaka kuwa ni pamoja na, kupanda kwa bei za vyuma katika soko la dunia unaosababisha upandaji wa gharama za uwekezaji katika kutoa huduma ya majisafi, uchakavu wa miundo mbinu ya kusambaza huduma ya maji,Ongezeko la watu mijini, uchafuzi wa vyanzo vya maji, uchomaji ovyo misitu na nyingine nyingi. Hata hivyo Dkt. Bilal alitoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana kwa karibu na serikali ili kukabiliana na changamoto tulizo nazo za utoaji huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka katika miji yetu.


Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa baadhi ya wadau wa masuala ya maji jinsi ya kupata majisafi kupitia vyombo vya kitaalamu.


Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Bilal akiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark J. Mwandosya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Hiroshi Nakagawa wakisiliza maelezo juu ya pampu ya maji iliyotengenezwa na watanzania kukidhi hali halisi ya mtanzania..



Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa vyeti na vikombe kwa washindi wa kutunza na kuhifadhi maji kutoka makampuni mbalimbali...


Picha ya pamoja na washindi kutoka makampuni mbali mbali

Ajali yaua 13: Ni wanamuziki wa kundi la Five Star Modern Taarab...




Kundi la wanamuziki wa Taarab kutoka Five Star Modern Taarab, wamepata ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Doha mkoani Morogoro wakitokea Kyela mkoani Mbeya kwa shughuli za muziki. Habari zinasema watu 13 wamefariki dunia katika ajali hiyo..
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amina

Monday, March 21, 2011

Shambulio la Kombora katika uwanja wa Gaddafi mjini Tripoli...



Pichani ni eneo la Gorofa tatu lililo haribiwa vibaya kwa shambulio la Kombora kutoka umoja wa majeshi yanayompinga Gaddafi. Eneo hilo lilikuwa likitumiwa na kiongozi wa Libya Maummar Gaddafi kurushia matangazo yake ya televisheni kabla ya kuharibiwa mapema Jumatatu. Waandishi wa habari waliitwa kutembelea eneo hilo na taarifa zinasema hakuna aliye umia katika shambulio hilo...

Uvumilivu unapofika kikomo....



Katika harakati za kumtoa kiongozi aliye itawala Libya kwa zaidi ya miaka 40, Maummar Gaddafi, wanawake wengi wamekuwa wakijifungia ndani ama katika mitaa wanayoishi kuhofia kufa, lakini si kwa mwanamke huyu ambaye kutokana na chanzo cha habari kutoka Reuters kinasema ni mpiganaji wa waasi wanaotaka kumtoa Gaddafi madarakani akifurahia vikosi vya Gaddafi kuondolewa katika mji wa Benghazi... LIBYA KAZI IPO!

MOTO wa STR8 MUSIC FREE STYLE 2011, all at Villa Park Mwanza


DJ SAMA All the way from STONE CLUB, akipokea zawadi baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kuchezea zile TURNTABLES... Hongera sana DJ SAMA


ERICK EMMANUEL akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza kwa free styles...


WASHINDI WA KWANZA: DJ SAMA from Stone Club akiwa na mshindi wa kwanza kwa free style Erick Emmanuel...


DJ D. Elisha akipokea zawadi baada ya kuibuka mshindi wa pili kwa upande DJz free styles...


Washiriki na waandaaji wa STR8 MUSIC FREE STYLE 2011 kwa pamoja baada ya mpambano kuisha...


DJ SAMA akionyesha ujuzi kwenye TURNTABLE...


DJ D. ELISHA akisababisha wakati wa mpambano wa DJz free styles..


ERICK EMMANUEL, akitoa dozi za free styles...


JAJEZ walikuwa makini wakifuatilia mpambano...


Msanii wa HIPHOP kutoka Jijini Arusha JO'MAKINI maarufu kama MWAMBA WA KASKAZINI ambaye pia ni mkali wa free style alikuwepo katika tukio akiwapa mzuka mashabiki wa mziki wa HIPHOP... ONE LOVE JO'MAKINI


Mashabiki wamepagawa... Shangwe za kutosha....

Thursday, March 17, 2011

JAPAN hali si shwari... Tuwaombee ndugu zetu!





Sprite Basketball Bonanza in Mwanza....


Pichani (waliokaa) ni timu ya mpira wa kikapu ya BUGANDO HEAT ambao waliibuka washindi wa kwanza katika Bonanza la mpira wa kikapu lilioandaliwa na kampuni ya vinywaji baridi kupitia kinywaji chake cha Sprite kwa kushirikiana na chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza - MRBA. Waliosimama ni viongozi wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza wakiwa na Bwana MZIYA (Watano kutoka kulia)ambaye Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu nchini - TBF.

Pichani ni SIMON CHERU mchezaji wa Bugando Heat na pia nahodha wa timu ya mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza akipokea zawadi ya mpira baada ya kupata ushindi wa mchezaji bora 'MVP' (Most Valuable Player) katika bonanza hilo.

SIMON CHERU akiwa katika michuano ya kupiga DUNK...


Pichani ni kijana ERICK JOHN akipokea zawadi ya mpira baada ya kupata ushindi wa kuwa mpiga DUNK bora wa kwanza katika bonanza hilo...ERICKanachezea klabu ya mpira wa kikapu ya BUGANDO WORRIERS.


ERICK JOHN akiwa hewani kuelekea golini kupiga DUNK.. Wenyewe wanaita Kusafiri hewani..

Pichani anaitwa TIMOTH NGALULA mchezaji wa klabu ya mpira wa kikapu ya BUGANDO HEAT akiwa hewani tayari kwa kupiga DUNK...


Anaitwa PASCAL MAGABE kijana anayesifika kwa kuruka kupita kiasi. Pichani akijaribu kupiga DUNK kwa kutumia mipira miwili...


MOSES JACKSON akisafiri hewani kupiga DUNK... Hawa vijana ni kama wamevishwa PISTON kwenye miguu...